UZEMBE NA UPOFU BANDIA SERIKALINI

Kwa muda wa miongo miwili nchi ya kenya imekua ikikumbwa na majanga tofauti ikiwemo,baa la njaa,mafuriko,na mashambulizi ya kigaidi ambayo yamepoteza mamia ya ya maisha ya wananchi wasio hatia. Ukweli halisi ni kwamba hata japo kuwa baadhi ya majanga hayatabiriki na hukumba nchi pasi na kutarajia ila ukweli ni kwamba serikali imezidisha uzembe na upofu bandia katika juhudi za kukabiliana na majanga haya mathalan shambulizi la kigaidi la WEST GATE NA CHUO KIKUU CHA GARISSA. Kulingana na ripoti ya kijasusi mwaka 2013 iliyofichuliwa na shirika la habari la CNN ni kwamba kenya ilionywa dhidi ya mashambulizi ya kigaidi lakini kitengo cha kijasusi hakikutilia maanani na kilichofuatia ni mauwaji ya wakenya wasio na hatia. https://makangayussuf.files.wordpress.com/2016/10/2013929152639826734_20.jpg?w=2924

Laiti serikali ingetahadhari mapema tusingeshuhudia mauwaji ya wakenya wenzetu lakini hayo hayakufanyika. Tuseme magaidi hawajulikani siku wala saa ya uvamizi wao na hata endapo watavamia kuna uwezekano wa baadhi ya wananchi kuponea.
BAA LA NJAA hili ndo janga na zimwi linalowala na kuwafyonza wakenya kina yakhe,wakenya walala hoi,wakenya wa pangu pakavu tia mchuzi, wakenya wa ntakula nini sio ntakula na nini. Njaa ni ugonjwa ambao endapo mnyama ama binadamu atakosa chakula hatima yake ni kifo tu tofauti na magaidi ambao wanaeza kosa kuwaona watu wengine wakati wa uvamizi na wakaponea. Kwa hili serikali imefeli asilimia 80%. Itakumbukwa kwamba mwaka jana serikali iliweza kutenga fedha kiasi cha shilingi bilion 15 ili kukabiliana na mafuriko yaliyokisiwa. Fedha hizo hazikutumika ipasavyo na zikazua mtafaruku serikalini. Baa la njaa ni janga linalo ikumba kenya takribani kila mwaka……..je serikali inakosaje kujipanga kukabiliana na janga hili kiasi cha kusababisha maafa ya wakenya?
https://makangayussuf.files.wordpress.com/2016/10/14713694_1260184087366901_7095677095273633834_n.jpg?w=900https://makangayussuf.files.wordpress.com/2016/10/14606536_2118949838331111_7196769736349213775_n.jpg?w=900. Itakumbukwa kwamba majuma kadha yaliyopita wabunge walijaribu kujikusanya na kujaribu kushurutisha serikali itangaze baa la njaa kama jangwa la kitaifa. Swali ni je mbona walizimbaa wakati huo wote mpaka sasa wananchi maji yamewafika shingoni ndo wapo mbioni kulazimisha serikali kuitangaza njaa kama janga la kitaifa,mbona hawakutayarisha na kupitisha mswaada utakao hakikisha kwamba majanga kama haya yanakabiliwa vilivyo pasi na wakenya wachochole kuumia? UZEMBE NA UPOFU BANDIA WA HALI YA JUU. https://makangayussuf.files.wordpress.com/2016/10/parliamentinsession.jpg?w=900

Advertisements

4 thoughts on “UZEMBE NA UPOFU BANDIA SERIKALINI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s