Watangazaji watano wanaopigania mziki wa kizazi kipya pasi na kutambuliwa juhudi zao.

Tenda wema uende zako!! Nadhani hii ndo itakua kauli wanayoitumia wakali hawa wanaoupigania mziki wa kizazi kipya . Ila kwa sasa wasanii wanaowapigania hawawatambui tena .

1.Mwinyi Kazungu Nyawa. Wanamuita superstar, mtetezi ama ukipenda yule tajiri wa mziki wa kizazi kipya. Ni mtangazaji ambaye amewainua wasanii tajika kimziki hapa nchini ambao walipata kusikika kwenye kipindi cha KETAU Express enzi hizo kwenye Radio ya KBC. Ila cha kushangaza ni kwamba baadhi yao wanamuona mtu wa kawaida na hata kususia interview zake.

kk

2.Mkali huyo wa mambo mseto Mzazi Willy M. Tuva mchango wake upo wazi kwenye mziki wa kizazi kipya inchini kenya ila hilo halitambuliwi kwani hata baada ya juhudi zake bado kuna baadhi ya wasanii bila haya wamekua wakimshambulia kwenye mitandao na kusema mtangazaji huyo ana kibri na anawakandamiza wasanii chipukizi.tuva

3. Gates Mgenge a.k.a The grandson. Ni mmoja wa watangazaji ambao kila kukicha anafanya kila awezalo kuona kwamba mziki wa kizazi kipya hasa wa pwani unapata nafasi kwenye soko kupitia kipindi cha MASHAVMASHAV UNIVERSITY Pwani Fm, ila wengine wao wakipata mwanya husepa na kutokomea Nairobi, Japo wengine wao hufulia na kurudi bila………..

gg

4. Tatu Amani .

tt

Sauti kama ilivyo sura yake vile!! Yeye huwa anachachawiza kwa sauti na hata kimziki ila hili watu wengi hawalioni akiwa nyuma bomba utatamani show isiishe ila ni kazi buree, wapo wanaomkashifu na kusema bidada huyo ana kibri, mnataka lipi walimwengu?

5. Sister Shanniez Saban a.k.a Aunt Virus

shan

Huyu naye anacheza ligi moja na Gates Mgenge maana wasanii anaowapata support wakitusua tu, hao ……!! mara wamefulia wanarudi tena.

Mgala muuwe na haki umpe, kibri dharau ni vyetu tuliumbiwa sisi binadamu na siku zote tabia itakua ya binadamu na wala si malaika, hawa watu hukosea lakini ukweli usemwe wanahitaji kupongezwa kwa juhudi zao.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s